Na Mwandishi wetu.
Mtoto Mchanga mwenye jinsi ya kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa wiki mbili anadaiwa kutelekezwa na mama yake mzazi ambaye hadi sasa hajafahamika mara moja ,akidai kuwa anahali mbaya kimaisha ya kumlea mtoto huyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Wilaya ya Musoma Mkoa wa Mara iliyotolewa na Kamanda wa Jeshi hilo Pius Lutumo imesema kuwa, tukio hilo limetokea June 9, 2025 majira ya saa 11: 30 jioni Katika njia inayoelekea stendi ya mabasi ya Bweri Katika manispaa ya Musoma Mkoani Mara, ambapo hadi sasa uchuguzi unaendelea ili kumbaini Mama Mzazi wa Mtoto aliyefanya tukio hilo
“Mama Mzazi wa Mtoto huyo aliacha ujumbe wa maandishi pembeni ya mtoto huyo uliosomeka kuwa ameshindwa kumlea mtoto huyo kwasababu yeye ni mwanafunzi “Alisema Kamanda LutumoJeshi hilo
limesema kuwa hadi sasa mtoto huyo ameifadhiwa katika kituo cha kulelea watoto Cha Bweri Center huku likitoa wito na kuwataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo ili kumbaini Mama Mzazi wa mtoto huyo na kumchukulia hatua kali za kisheria dhidi yake.
#NTTUpdates