Na Mwandishi wetu.
Baada ya kiungo mshambuliaji Bora wa muda wote wa Mabingwa watetezi wa EPL, Manchester City na timu ya Taifa ya Ubelgiji, Kevin De Bruyne (33), kutangaza kuondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huku baada ya kuwatumikia kwa miaka 10, uongozi wa klabu hiyo umepanga kutengeneza sanamu la nyota huyo ili kuenzi mchango wake ndani ya kikosi hicho.
“Nitaweka dau la pesa nyingi sana! Hiyo ni hakika, Lakini sijui … Lakini bila shaka, anastahili kuwa katika kiwango hiki”.
Aliizungumza Pep Guardiola Kocha wa Manchester City alipoulizwa na Waandishi wa habari kama klabu hiyo Ina mpango wa kumtengenezea sanamu De Bruyne.
De Bruyne ambaye alijiunga na miamba hiyo ya Uingereza mwaka 2015 akitokea VfL Wolfsburg ya Ujerumani amekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikosi hicho baada ya kusaidia Manchester City kutwaa mataji 6 ya EPL, taji moja la UEFA na ubingwa wa klabu bingwa ya Dunia.
Sanamu hilo linatarajiwa kujengwa nje ya uwanja wa Etihad ili kukumbuka mchango wa nyota huyo ambaye ataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
#NTTupdates