Na Mwandishi wetu.
Mambo yameendelea kuwa magumu kwa mashetani Wekundu Manchester United baada ya kupoteza mchezo wao wa 18 wa ligi kuu Uingereza (EPL) hapo jana dhidi ya Chelsea kwa kichapo cha goli 1-0.
Vijana wa Ruben Amorim wameweka rekodi mbaya ya kushindwa kupata ushindi kwenye michezo 15 ndani ya msimu mmoja huku klabu hiyo ikitajwa kuwa ndio Man United yenye matokeo mbovu zaidi kuwahi kutokea.
Kichapo hicho kinaifanya Manchester United kusalia nafasi ya 16 kwenye msimamo la ligi ya EPL baada ya kucheza michezo 37 wakivuna alama 39 tu.
Mara ya mwisho kwa Manchester United kubeba taji la ligi kuu EPL ilikuwa msimu wa 2012-2013 chini ya Sir Alex Ferguson.
#NTTupdates