Na Mwandishi wetu, Dodoma.
WAZIRI wa fedha Dkt.Mwigulu Nchemba amesema Tanzania imekusudia kuanza kutumia michezo ya kubahatisha kamari, kwaajili ya kukusanya fedha zinazotumika kulipia bima za watu wasiojiweza na makundi maalum.
Ameyasema hayo leo Juni 13,2024 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti kuu ya Serikali katika mwaka wa fedha 2024-2025. Dkt.Mwigulu amesema hilo litawezekana baada la kutoza asilimia 10 kwenye thamani ya dau la kamari kwenye michezo ya kubahatisha.
Pia ametangaza asilimia 10 katika kila ada ya matangazo ya biashara za michezo ya kubahatisha yanayotangazwa kupitia vituo vya television redio na uchapishaji.
Mwigulu amesema kufuatia uanzishwaji kwa tozo hizo Serikali inatarajia kukusanya kiwango kikubwa cha fedha.
#NTTupdates