Na Mwandishi wetu.
Mchezo mkubwa wa derby nchini Kenya maarufu kama Mashemeji Derby kati ya AFC Leopards SC na Gor Mahia SC utapigwa leo kwenye dimba la Nyayo jijini Nairobi majira ya saa 10:00 Jioni.
Mechi hiyo ambayo ilighairishwa zaidi ya mara mbili na shirikisho la soka Kenya kutokana na kukosekana kwa uwanja baada ya uwanja wa Nyayo kuwa kwenye matengenezo.
Gor Mahia SC ambayo ipo nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kuu Kenya wakiwa na alama 42 baada ya kucheza michezo 23 huku AFC Leopards SC wakiwa nafasi ya 5 baada ya kucheza michezo 23 wakivuna alama 36.
#NTTupdates