Na Mwandishi wetu.
Matajiri wa Chamazi Azam FC, imefikia makubaliano na Mkongomani Jean Florent Ibenge (63), kukinoa kikosi hicho akichukua nafasi ya Rachid Touassi aliyemaliza mkataba wake ndani ya klabu hiyo.
Ibenge ambaye anajiunga na Azam FC akitokea Al Hilal ya Sudani amekubali ofa ya klabu hiyo na atakiongoza kikosi hicho msimu ujao.
Uongozi wa Azam FC unaamini uzoefu mkubwa alikuwa nao Ibenge ni chaguo sahihi kwa ajili ya michuano ya kimataifa ya kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) kwa msimu ujao pia anazijua vyema mahasimu wao wawili ambao ni klabu ya Simba na Young Africans kwenye kupambania ubingwa wa ligi kuu.
#NTTupdates