×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MBEUMO HAUZWI EPUKA MATAPELI

Na Mwandishi wetu.

Meneja wa Kikosi Cha Brentford Thomas Frank ameweka wazi kuwa mshambuliaji wa kikosi hicho Bryan Tetsadong Marceau Mbeumo (25) raia wa Cameroon hatoenda popote kwenye dirisha dogo la Januari, kwa sababu bado klabu hiyo inahitaji huduma ya mshambuliaji huyo.

Mbeumo, ambaye amekuwa akisakwa na vilabu kadhaa barani Ulaya kutokana na uwezo wake ambao ameuonyesha msimu huu ndani ya Brentford ambapo mpaka sasa amecheza michezo 25, akifunga magoli 13 na assist 4 kwenye michuano yote ambayo Brentford imeshiriki msimu huu hadi sasa.

Arsenal, Chelsea na Aston Villa ni miongoni mwa Vilabu vilikuwa vikihusishwa kumuhitaji mchezaji huyo.

#NTTupdates