×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MBUEMO ” HII NDIO TIMU YA NDOTO YANGU”

Na Mwandishi wetu.

Mshambuliaji mpya wa Mashetani Wekundu Bryan Mbuemo, mwenye umri wa miaka 25 raia wa Cameroon, ameweka wazi kuwa toka zamani ndoto yake kubwa ilikuwa kujiunga na klabu ya Manchester United.

“Mara tu nilipojua kuna fursa ya kujiunga na Manchester United, ilibidi nichukue nafasi hiyo kusaini klabu ya ndoto zangu.

Hii ndiyo timu ambayo nilivaa shati lake wakati nakua”Alizungumza Mbuemo baada ya kusaini mkataba ndani ya klabu hiyo.

Man United imemsajili mshambuliaji huyo akitokea klabu ya Brentford kwa ajili ya kuimarisha safu yao ya ushambuliaji ambapo walitoa dau la zaidi ya Paundi Milioni 70 ili kuwania saini yake huku wakimpatia mkataba wa miaka 5 Hadi 2030, kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mwingine.

Nyota huyo ambae amekabidhiwa jezi namba 19, alikuwa na wakati mzuri msimu uliopita akiwa Brentford ambapo alicheza michezo 38 akifunga magoli 20 na kutoa assist 7 kwenye ligi kuu ya Uingereza (EPL).

#NTTupdates