×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MIRADI YA BILIONI 79 YAPITISHWA NA MWENGE WA UHURU 2025 DSM

Na Mwandishi wetu.

Mwenge wa Uhuru 2025 ulianza kukimbizwa katika Mkoa wa Dar es salaam Juni 1, 2025 ukianza Wilaya ya Temeke, Juni 2, 2025 Kigamboni, Juni 3, 2025 Ilala, Juni 4, 2025 Kinondoni na Juni 5,2025 umehitimishwa Wilaya ya Ubungo.

Katika Mkoa wa Dar es Salaam Mbio za mwenge wa Uhuru zikiongozwa na Ndg Isumail Ali Ussi Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ameongoza kuukimbiza Mwenge huo umbali wa Km 357.03 ukitembelea, kukagua, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani zaidi ya Bilioni 79. ambapo miradi yote imepitishwa na Mwenge wa Uhuru hakuna mradi uliokataliwa.

Aidha Mwenge wa Uhuru ukiwa unakimbizwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa umeendelea kuelimisha jamii na kuwahamasisha wananchi kupitia kaulimbiu ya mwaka huu isemayo “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu” pamoja kuhamasisha wananchi mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Malaria, Rushwa na mapambano dhidi ya Madawa ya kulevya.

Mwenge wa Uhuru 2025 leo Juni 6, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameukabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambako utaendelea kutembelea, kukagua, kuweka Jiwe la msingi na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

#NTTupdates