×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MKAZI WA ARUSHA AREJESHEWA SHAMBA LAKE KUPITIA KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA

Na Mwandishi wetu.

Mkazi wa Kijiji cha Olevolosi Kata ya Kimnyaki Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha anayefahamika kwa jina la Joseph Mollel kupitia Kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia ( Samia legal Aid Campaign) leo Aprili 4, 2025 amefanikisha kurejesha shamba lake lililokuwa rehani kwa muda mrefu.

Bw. Mollel ameishukuru Serikali ya Dkt. Samia kwa kuendelea kuwajali wananchi wake kwa kuwatatulia changamoto mbalimbali zinazowakabili kupitia Wizara mbalimbali kitu ambacho kinawapa faraja wao kama wananchi.

Aidha, ameeleza namna ambayo amenufaika kwa msaada huo wa kisheria alioupata kwani imemsaidia kurejesha shamba lake ndani ya muda mfupi tofauti na mwanzo alivyokuwa akizungushwa.

Naye, Losiyaki Mollel ambaye alidai kuwa shamba hilo ni mali yake kutokana na Bw. Joseph kuliweka rehani na kushindwa kumlipa fedha alizokuwa amemkopesha kiasi cha fedha sh. 490,000 ambapo Bw. Joseph amekiri kupokea fedha hizo.

Kwa upande, Wakili Gift Ayo ambaye amekiri kufanya utatuzi wa mgogoro huo kati ya Bw. Joseph Mollel na Bw. Losiyaki Mollel ambaye alikuwa akidai shamba hilo ni mali yake kurudishiwa fedha zake na shamba hilo kurudishwa kwa mmiliki halali.

#NTTupdates.