×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MNYAMA ACHAPIKA MISRI

Na Mwandishi wetu.

Mchezo wa kwanza hatua ya robo fainali kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) umemalizika kwenye uwanja wa Suez nchini Misri kati ya Al Masry dhidi ya Simba SC na kushuhudia wenyeji wakitakata baada ya kupata ushindi wa magoli 2-0

Magoli ya mchezo kwa Al Masry yamefungwa na kiungo mshambuliaji Abderrarhim Deghmoum dakika ya 16′ huku goli la pili likifungwa na John Okoye dakika ya 89′ na kuwafanya Al Masry kutanguliza miguu mmoja hatua ya nusu fainali.

Simba SC italazimika kupata ushindi wa kuanzia magoli 3 na kuendelea huku wakitakiwa kuwazuia Al Masry wasipate goli la ugenini kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ili kufuzu kwenye hatua ya nusu fainali ambayo imekuwa ndoto ya Mnyama Simba SC kwa zaidi ya misimu mitano kwenye michuano ya kimataifa.

#NTTupdates