Na Mwandishi wetu.
Kikosi cha Simba SC kimeendelea na Maandalizi yake ya mchezo wa Mkondo wa kwanza wa Fainali kombe la shirikisho Afrika (CAFCC), dhidi ya RS Berkane baada ya kuwasili salama jijini Casablanca nchini Morocco.
Simba SC imesafiri na wachezaji 25 na wameweka wazi kuwa ndoto yao ni kubeba taji hilo na kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza kutoka ukanda wa Afrika Mashariki kubeba taji hilo.
Simba SC itacheza na RS Berkane siku ya Jumamosi Mei 17, 2025 kwenye dimba la Berkane Municipal uliopo kwenye mji wa Berkane nchini Morocco huku mchezo wa Mkondo wa pili utapigwa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, Mei 25, 2025 na mshindi wa matokeo ya jumla atabeba taji hilo.
#NTTupdates