Na Mwandishi wetu.
Saa chache zimesalia kushuhudia mchezo mkali wa Mkondo wa kwanza wa Fainali kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) kati Jeshi la Machungwa RS Berkane dhidi ya Mnyama Simba SC kwenye dimba la Berkane Municipal nchini Morocco.
Simba SC imejipanga kupata ushindi kwenye mchezo huo wakitaka kuweka historia ya kuwa klabu ya kwanza kutoka Afrika Mashariki na kati kubeba taji hilo.
Berkane ambao ndiyo Mabingwa wa ligi kuu Morocco wamejipanga pia kuumaliza mchezo huo nyumbani kwao kabla ya kuja machinjioni Benjamin Mkapa ambapo Simba SC wamekuwa wakifanya vizuri zaidi kwenye michuano mikubwa Afrika.
#NTTupdates