×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MOHAMED HUSSEIN NI MALI HALALI YA WANANCHI

Na Mwandishi wetu.

Aliwahi kuwa Nahodha wa kikosi Mnyama Simba SC kwa muda mrefu Mohamed Hussein Zimbwe Jr pia akijulikana kama ” Tshabalala” ametambulishwa rasmi na Mabingwa mara nyingi zaidi wa ligi kuu Tanzania bara Young Africans SC kuwa mchezaji wao mpya kuelekea msimu ujao wa 2025/2026.

Zimbwe ambaye aliwatumikia Simba SC kwa misimu 11 amejiunga rasmi na Young Africans SC akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Simba SC na kushindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya.

Young Africans SC inaendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao huku nyota huyo anatarajiwa kuungana na wachezaji wenzake baada ya kumalizika kwa michuano ya CHAN 2024.

#NTTupdates