Na Mwandishi wetu.
Winga wa kimataifa wa Hispania na klabu ya Atletic Bilbao, Nico Williams Arthuer (22) amekataa ofa ya Mabingwa wa ligi kuu Hispania (La Liga) FC Barcelona na kuamua kusaini kandarasi mpya na klabu yake itakayomuweka klabuni hapo Hadi 2035.
“Linapokuja suala la kufanya maamuzi, kwangu jambo la muhimu zaidi ni kusikiliza moyo .””Niko mahali ninapotaka kuwa, na watu wangu, Hii ni nyumba yangu.
“Nico Williams aliweka wazi maneno hayo baada ya kusaini kandarasi yake mpya huku akiikataa ofa ya FC Barcelona kwa mara ya pili mfululizo na kuwashangaza watu wengi kwa nyota huyo kukataa kujiunga na klabu hiyo.
#NTTupdates