Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina leo Juni 20 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti kuu ya Serikali amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba aziondoe baadhi ya ibara katika hotuba yake ya bajeti kuu au atolee ufafanuzi hasa katika suala la katazo la kuzuia kufungwa kwa biashara kwa aina yoyote ile hata kama mfanyabiashara hajazingatia sheria.
Kadhalika Mpina amezungumzia kuhusu suala la ukusanyaji wa mapato na kusema Serikali haijakusanya zaidi ya Trillion 15,huku akisema yote hiyo ni kwasababu ya usimamizi mbovu wa mapato.