×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MPINA ASHINDA KESI DHIDI YA INEC

Na Mwandishi wetu .

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, imetoa uamuzi unaompa uhuru mwanasiasa wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, kuendelea na mchakato wa kurejesha fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika uamuzi uliosomwa na Jaji Abdi Kagomba, Mahakama imeamua kuwa zuio lililotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) tarehe 27 Agosti 2025 halikuwa halali kisheria, kwani lilikiuka haki ya msingi ya kusikilizwa kwa upande wa Mpina na chama chake.

Shauri hilo liliwasilishwa na Bodi ya Wadhamini ya ACT Wazalendo pamoja na Luhaga Mpina dhidi ya INEC na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mahakama imekubaliana na hoja za walalamikaji kuwa hatua ya kuzuia urejeshaji wa fomu bila kuwapa nafasi ya kujieleza ilikuwa ni ukiukwaji wa Katiba na misingi ya haki.

Kutokana na maamuzi hayo, Mahakama imeamuru Mpina apewe nafasi ya kurejesha fomu yake mara moja ili aweze kuendelea kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi.

Uamuzi huu umetafsiriwa kuwa ni ushindi mkubwa kwa misingi ya haki, uwazi na usawa katika michakato ya kidemokrasia nchini.

#NTTupdates