×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MRITHI WA ZIMBWE HUYU HAPA

Na Mwandishi wetu.

Klabu namba 5 kwa Ubora barani Afrika, Simba SC imethibitisha kukamilisha usajili wa nyota, Naby Camara raia Guinea ikimpatia mkataba wa miaka miwili kuwatumikia wazee wa Ubaya Ubwela.

Camara mwenye umri wa miaka 23, ana uwezo mkubwa wa kucheza kama mlinzi wa kushoto na pia kiungo mkabaji, amejiunga na Simba SC baada ya kumaliza mkataba wake na Al Waab ya nchini Qatar.

Simba SC wanaamini Camara atakuwa mbadala sahihi hasa eneo la kushoto baada ya kuachana na aliyekuwa Nahodha wao Mohamed Hussein na Valentine Nouma ambao wote walikuwa wakicheza kama walinzi wa kushoto.

#SimbaSC

#NTTupdates