Na Mwandishi wetu, Dodoma.
Serikali imewahimiza vijana kote nchini kutumia mitandao ya kijamii kama nyenzo ya kujiletea maendeleo ya kiuchumi badala ya kuitumia kwa mambo yasiyo na tija.
Kauli hiyo imetolewa leo Juni 11,2025 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari , Utamaduni ,Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Jengo la ofisi ya Wizara hiyo Mtumba Jijini Dodoma.
Msigwa amesema sheria itachukua mkondo wake kwa vijana watakaojihusisha na ukiukwaji wa maadili ya kitanzania huku akidai kipindi hichi cha uchaguzi mihemko na upotoshaji unakuwa mwingi ni vyema vijana hao kukwepa kutumika na wanasiasa.
“Naomba niwambie vijana tumieni mitandao hii kujifunza acheni kutumika kutukana serikali kwani sheria ipo vyombo vya dola vipo hivyo yeyote ataye kiuka sheria itachukua mkondo wake.”
“Wengi tunao wakamata wanasema nilikua sijui lakini kutokujua siyo sababu ya kufanya usichukuliwe hatua naomba niwaonye mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mihemuko imekua mingi hivyo vijna jiepusheni kutumika na watu kutoa matusi mitandaoni ama kukashifu watu” amesema Msigwa
#NTTupdates