Na Mwandishi wetu.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa, hatimaye amekabidhi Ofisi Mkuu mpya wa Wilaya hiyo Ndg. Joseph Mkude aliyeteuliwa mnamo Januari 25, 2025 na Mhe. DKt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mtahengerwa aliyedumu katika ofisini ya Ukuu wa Wilaya ya Arusha kwa miaka miwili pekee tangu Januari 25, 2023 alipoteuliwa rasmi katika nafasi hiyo mpaka Januari 25, 2025 baada ya kutenguliwa katika nafasi hiyo na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mtahengerwa amewashukuru watumishi wenzake kwa ushirikiano wa karibu waliompatia kwa muda wote tangu alipoingia Ofisini hadi wakati anaondoka ndani ya ofisi hiyo huku akisema ataendelea kushirikiana nao pale ambapo watahitaji uwepo wake kwa lengo la Kujenga Taifa.
Kwa upande wake, DC Mkude ambaye amepokea ofisi kutoka kwa Mtahengerwa amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kumuamini na kuahidi kutomuangusha kwa kuitumikia nafasi hiyo kwa utumishi uliotukuka.
Aidha, Mkude amewashukuru watumishi wenzake kwa mapokezi mazuri waliyompatia na kuomba ushirikiano uendelee katika utekelezaji wa majukumu yake mapya ndani ya Wilaya ya Arusha.
#NTTupdates.