Na Mwandishi wetu.
Matajiri wa Chamazi Azam FC imemtambulisha rasmi Kocha wao mpya Florent Ibenge (63) raia wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo kuwa Kocha wao mkuu kwa mkataba wa miaka 2 kukinoa kikosi hicho.
Ibenge ambaye ni mwalimu mwenye wasifu mkubwa barani Afrika akizifundisha vilabu vikubwa kama RS Berkane, As Vita, Al Hilal Omdurman ya Sudan pamoja na Timu ya Taifa ya DRC ameahidi kufanya vizuri ndani ya Azam FC huku akizigusia vilabu vya Kariakoo ambao ni Simba SC na Yanga SC.
#NTTupdates