×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MUIGIZAJI CARINA AFARIKI DUNIA

Na Mwandishi wetu.

Muigizaji wa filamu nchini Tanzania Hawa Ibrahim “Caroline” amefariki dunia leo Aprili 15, 2025 nchini India ambapo alipelekwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Hawa alitarajiwa kurejea nchini leo baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa wa utumbo ambao ulikuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

Hawa alisafiri kwenda India kwa msaada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alimchangia muingizaji huyo fedha za matibabu baada ya kusumbuliwa na tumbo kwa zaidi ya miaka 10 likitoa usaha na kupeleka maumivu makali kwa mrembo huyo.

Inna Lillah Wainna Ilaihi Rajiuun.

#NTTUPDATES