Na Mwandishi wetu.
Klabu ya Hapoel Ramat Gan inayoshiriki ligi kuu ya Israel, imetangaza kumsajili mshambuliaji Kennedy Musonda (30) raia wa Zambia.
Kennedy Musonda, amejiunga na klabu hiyo kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na mabingwa kihistoria wa ligi kuu ya Tanzania Bara Young Africans SC.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram nyota huyo amewashukuru viongozi na mashabiki wa klabu hiyo kwa upendo wao wakati wote akiwatumikia na kufanikiwa kubeba mataji yote makubwa ndani ya Tanzania.
#NTTupdates