Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda amesema changamoto ya upatikanaji wa maji katika mkoa huo imepungua kwa kiasi kikubwa kulinganisha na hapo awali kwani huduma hiyo inatolewa na taasisi tatu amabazo ni MWAUWASA, SEUWASA na RUWASA hili kuhakiksisha wananchi wanapata huduma ya maji ya uhakika.
Amesema ongezeko la mradi wa maji umeongezeka kwa asilimia 57 kwa mwaka 2021 hadi asilimia 85 2025 ambapo ni sawa ongezeko la asilimia 27 ambapo kwa wilya ya misungwi imeongeza kutoka asilimia 12 hadi 90, kwa nkoa wa magu kutoka asilimia 55 hadi 93.3, wilaya ya sengerema kutoka 61 hadi 92, huu kwa wilaya ya Ilemela 81 adi 90, kwa wilaya nyamagana kutoka asilimia 59 hadi asilimia 78, wilaya ya ukerewe kutoka asilimia ukerewe 59 hadi asilimia 81 na kwa wilaya ya kwimba imeongezeka kutoka asilimia 67 hadi asilimia 78.
Mtanda ameongeza kuwa mradi wa maji Buhongwa, kishiri, Usagara na Kisesa tayari imetengewa fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 49.2 na hadi sasa miradi imefikia asilimia 16 huku kwa mradi wa usambazaji maji kwa maeneo ya Luchelele umefikia asilimia 85 katika utekelezaji wake.
Kuhusu hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa Mkoa wa Mwanza amesema kwa mwaka 2021 imeongezeka kutoka asilimia 57 hadi asilimia 77 kwa mwaka 2025 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 20 huku kwa hali ya ukamilishaji wa miradi ya maji katika maeneo ya vijijini mkoa umekamilisha jumla ya miradi 80 yenye thamani ya shilingi Bilioni 100.3 kupitia mamlaka ya maji Vijijini.
#NTTUpdates