×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MWAROBAINI WA TATIZO LA NJAA TANZANIA.

 MAKAMU wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philip Mpango amesema uwekezaji unaofanywa na serikali katika sekta ya Umwagiliaji unaenda kuandika historia ya kumaliza tatizo la njaa nchini na kulijengea Taifa heshima kupitia uwepo wa chakula cha kutosha.

 Amesema anaridhishwa  na kazi kubwa inayofanywa  na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji chini ya Wizara ya kilimo hivyo wananchi wawe tayari kuipokea miradi hiyo mikubwa sekta ya umwagiliaji itakayomaliza tatizo la uhaba wa chakula na kuimarisha kilimo cha uhakika nchini. 

 Dkt. Mpango amesema hayo leo katika ziara yake Mkoani Dodoma wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi katika ujenzi wa Shamba la Pamoja la Dkt. Samia Suluhu Hassan (Dkt Samia Suluhu Hassan Block Farm) ambao unaotekelezwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ukiwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 21.7

 “Hapa Dodoma kuna salamu ya Mkuliachi ambayo ni salamu na inamaanisha njaa, niwahakikishie kuwa hiyo salamu inaenda kuisha  kupitia uwekezaji unafanywa na serikali katika miradi hii mikubwa ya umwagiliaji inaenda kuandika historia ya kumaliza tatizo la njaa nchini na kulijengea Taifa heshima ya uwepo wa chakula cha kutosha. 

 “Niwashukuru wananchi wa maeneo ya mradi kwa kuridhia kutoa ardhi yao na kazi kubwa inayofanywa na Tume chini ya Wizara ya kilimo katika kufanikisha miradi hii,”alisema. 

 Aidha Dkt. Mpango, amesisitiza kuwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji,  na inafanya kazi kubwa na hatua hiyo ndio maana ya kubadili mifumo sekta ya kilimo na kuwa na kilimo chenye tija  na cha uhakika. 

“Nawapongeza sana,hili litakuwa ni eneo la mfano na mashamba haya yawe mashamba darasa,elimu ya Kilimo itolewe hadi kwa vijana hususani vitendo siyo maneno”

 Alitumia fursa hiyo kusifu hatua ya mradi huo kuhusisha ujenzi wa kituo cha afya na barabara  yenye urefu wa zaidi ya kilomita 18.8 umbapo ujenzi huo unatekelezwa na Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

#NTTupdates