Na Mwandishi wetu.
Mwenge wa Uhuru mwaka 2025, umezindua Ofisi ya kijiji cha Ngulu kilichopo kata ya Kwakoa Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni hatua za Serikali za kuboresha mazingira ya watumishi katika utendaji kazi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Julai 1, 2025 kiongozi wa mbio za Mwenge, Ismail Ali Ussi amesema, Serikali imedhamiria kuboresha mazingira ya watumishi ili wananchi waweze kupata huduma iliyo bora kwa haraka na kwa wakati husika.
Aidha, amewataka watumishi watakaofanya kazi katika eneo hilo kufanya kazi kwa uwaminifu na kwa haraka ili kuwasaidia wananchi katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zitakazokuwa zikiwasilishwa Ofisini hapo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mwaga Bi. Rukia amesema kuwa kwasasa wananchi wa eneo hilo wataweza kutatuliwa matatizo yao kwa haraka na kwa wakati kutokana na kukamilika kwa ofisi hiyo kwani hapo awali kulikuwa na ofisi isiyokidhi mahitaji muhimu yanayotakiwa katika utendaji wa kazi.
Akisoma taarifa ya mradi huo, Bi. Angela Kilawe amesema hadi kukamilika kwa jengo la Ofisi hiyo jumla ya kiasi cha shillingi million 56 zimetumika.
#NTTupdates.