×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

MWILI WA MTOTO WA MIAKA (4) WAOKOTWA UKIWA HAUNA BAADHI YA VIUNGO DODOMA.

Na Mwandishi wetu, Dodoma.

MTOTO Telesphore Mwakalinga mwenye umri wa miaka minne amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya mwili wake kukutwa jirani na nyumba yao, ukiwa hauna baadhi ya viungo ikiwemo mkono pamoja na sehemu za siri.

Mtoto huyo alikuwa anaishi na familia yake katika eneo la nyumba 300 lililopo Kisasa Jijini Dodoma, na mauti yamemfika baada ya kupotea nyumbani kwao majira ya 12 jioni na kupatikana saa nne usiku akiwa amefariki dunia.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyumba 300 Donatha Zitatu akizungumza na NTT Media msibani hapo amesema alipata taarifa za kupotea kwa mtoto huyo jana majira ya saa kumi na mbili asubuhi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Theopista Mallya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jana usiku baada ya kutokea kwa tukio hilo alituma polisi ambaye alipofika katika eneo hilo aliona mbwa akiwa na kitu, jambo ambalo lilimfanya kusogelea karibu na kumuona mtoto huyo.

Amesema kwa hivi sasa hawawezi kusema kuwa mtoto huyo aliuawa ama vinginevyo hadi hapo watakapopata uhalisi wa tukio hilo baada ya uchunguzi kukamilika.

Mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na unatarajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Kasulu Kigoma kwa mazishi.

#NTTupdates