Na Mwandishi wetu.
Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba SC, Mzee Hassan Dalali “Field Marshal” , ametoa onyo kali kwa wale wote watakaopanga kuihujumu Simba SC, kwenye mchezo wa Mkondo wa pili wa Fainali kombe la shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya RS Berkane ya Morocco, siku ya Jumapili Mei 25, 2025 utakaopigwa kwenye dimba la New Amaan Complex Visiwani Zanzibar.
“Tunazo taarifa za watu ambao wamepanga kuihujumu Simba SC ikose Kombe, Uwe ndani au nje ya Simba ikitokea tunalikosa Kombe uwanjani hautoki hiyo Jumapili.
Huku usije nyau wewe” “Mwaka 1993 mgeni alikuwa Mwinyi kikombe kikaondoka, Jumapili mgeni tena Mwinyi alafu kikombe kiondoke hatukubali, Simba tunawakilisha nchi, mtu akitufanyia ubaya anahujumu nchi.”“Vijana hili kombe wanalitaka.
Tuwape ushirikiano kwa kuwashangilia muda wote uwanjani. Tuna timu nzuri sana njooni tushangilie timu yetu”.
Mzee Dalali ameyasema hayo kwenye uzinduzi wa hamasa katika viwanja vya Mnazi mmoja Visiwani Zanzibar.
#NTTupdates