Na Mwandishi wetu.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Serie A nchini Italy, SSC Napoli wameingia sokoni kusaka mshambuliaji mpya baada ya mshambuliaji tegemezi wa kikosi hicho, Romelu Lukaku Bolingoli kupata majeraha ya misuli yatakayo muweka nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi 3.
Lukaku mwenye umri wa miaka 33 aliumia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Olympiacos na kupelekea klabuni hiyo kuingia sokoni kwa lazima baada ya ripoti ya madaktari kuonyesha nyota huyo atakaa nje kwa muda mrefu.
Klabu ya Napoli wametuma ofa kwa Manchester United wakihitaji huduma ya mshambuliaji Rasmus Hojlund baada ya ofa ya awali ya Joshua Zirkzee kugonga mwamba