Na Mwandishi wetu.
Wachimba dhahabu kutoka Chunya jijini Mbeya, Ken Gold FC wameshuka daraja rasmi na kurejea ligi ya Championship ambayo walibeba ubingwa msimu uliopita baada ya kupokea kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa Coastal Union kwenye mchezo wa ligi kuu NBC uliopigwa kwenye dimba la Mkwakwani Tanga.
Ken Gold FC ambayo imeweka rekodi ya kusalia nafasi ya mwisho toka ligi kuu NBC msimu 2024/2025 inaanza mpaka sasa wanashuka daraja wakiwa na alama 16 baada ya kucheza michezo 27.
Licha ya kufanya usajili wa wachezaji wengi wenye uzoefu kwenye dirisha dogo la usajili lakini wameshindwa kuibaki timu hiyo ligi Kuu.
#NTTupdates