Na Mwandishi wetu.
Baada ya Mabingwa watetezi wa Saudi Pro League, Al Hilal ya Saudi Arabia kusitisha mkataba na winga wao wa kushoto, Neymar da Silva Santos Junior (32) raia wa Brazil, kutokana na majeraha na kutokuwa na kiwango Cha kuridhisha kwenye klabu huyo.
Neymar yupo mbioni kurejea kwenye timu yake ya utotoni na iliyomleta kwenye ramani ya soka Santos ya nchini Brazili ili kumalizia safari yake ya soka baada ya kuwa na wakati mgumu kupata timu kwenye ligi Tano Bora kutokana na majeraha yanayomsumbua.
Neymar alijiunga na Al Hilal mwaka 2023 na ameitumikia klabu hiyo kwenye michezo 7 pekee, akifunga goli 1 na kutoa assist 3 toka ajiunge na klabu hiyo na kupelekea matajiri wa klabu hiyo kumpa mkono wa kwa heri.
Neymar anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji wa muda wote wa timu ya Taifa ya Brazil akiwa na magoli 79 kwenye michezo 128 akifuatiwa na Pelle mwenye magoli 77.
Pia Neymar ndiye mchezaji pekee kutoka Brazil kufunga magoli mengi kwenye ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) akiwa na magoli 43 kwenye michezo 81.
@FabrizioRomano
#NTTupdates