×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

“NIMEPOKEA KWA MASIKITIKO MAKUBWA KIFO CHA SPIKA MSTAAFU NDUGAI” RAIS SAMIA

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Job Yustino Ndugai, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninatoa pole kwa familia, wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi, watumishi wa Bunge na Wabunge wote aliotumikia nao akiwa Spika wa Bunge letu, wananchi wa Kongwa, ndugu jamaa na marafiki.

Tuungane pamoja kumuombea kwa Mwenyezi Mungu na kuwaombea familia, ndugu, jamaa na marafiki uvumilivu, faraja na moyo wa ibada katika kipindi hiki kigumu.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.”

#NTTupdates