Na Mwandishi wetu.
Matabibu wa klabu ya Young Africans wamewatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kuhusu majeraha ya mshambuliaji Prince Dube ambayo aliyapata jana kwenye mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya wajelajela Tanzania prisons.
“Mchezaji Prince Dube amepata majeraha ya nyama za paja wakati wa mchezo dhidi ya Tanzania Priso sasa anaendelea na matibabu ya awali, pia ataweza kuimarika kwa michezo ijayo”.
Amesema Moses Ututu daktari wa klabu ya Yanga ikiielezea hali ya mshambuliaji huyo.
Mshambuliaji huyo ambaye hakuanza vyema mwanzoni mwa msimu huu amekuwa na mchango mkubwa ndani ya kikos Cha Young Africans SC akifunga magoli 13.
#NTTupdates.