Na Mwandishi wetu.
Baada ya kumalizika kwa michuano ya Ngao ya jamii, ikiwa ni ishara ya ufunguzi rasmi wa ligi kuu NBC 2024/2025, wana Tip Lindanda Pamba Jiji FC, watacheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Tanzania prisons ( Wajelajela) baada ya miaka 23 kupita.
Pamba jiji FC, chini ya Kocha Goran Kopunovic ametamba kuwa kikosi chake kipo tayari kucheza na kupata ushindi dhidi ya Tanzania prisons.
Tanzania prisons mbayo inafundishwa na Kocha wa zamani wa Pamba Jiji FC, Mbwana Makata ambaye aliisaidia klabu hiyo kupanda daraja baada ya miaka 23.
Mchezo utapigwa majira ya saa 10:00 alasiri kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, ambapo Pamba Jiji FC imewaomba Wananchi wajitokeze kwa wingi kuwashangilia.
#NTTupdates