×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

PATACHIMBIKA!!

Na Mwandishi wetu.

Leo ndio leo kwa Wananchi Young Africans SC, kuamua kutinga hatua ya robo fainali ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) au kuondolewa rasmi kwenye mashindano hayo msimu huu 2024/2025.

Young Africa SC, wataingia dimbani kucheza mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) dhidi ya MC Alger kutoka Algeria kwenye dimba la Benjamin Mkapa Dar es Salaam majira ya saa 10:00 Jioni ili kuamua hatma yao kwenye michuano hiyo.

Young Africans SC, ambao wana alama 7 nyuma ya MC Alger wenye alama 8 wanalazimika kushinda mchezo huo ili kupata alama tatu muhimu zitakazowawezesha kufuzu robo fainali ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL kwa mara ya pili mfululizo.

#NTTupdates