Na Mwandishi wetu.
Historia imeandikwa kwa klabu ya Al Hilal SC inayoshiriki ligi kuu ya Saudi Arabia (Saudi Pro League) baada ya kupata ushindi wa magoli 4-3 dhidi ya Manchester City kwenye michuano ya kombe la Dunia ngazi ya vilabu (FIFA) nchini Marekani.
Ushindi huo umewafanya Al Hilal kutinga hatua ya robo fainali ambapo watakutana na Flumenense ya Brazil kusaka nafasi ya kutinga nusu fainali ya kombe hilo.
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola alionekana kuvurugwa na kumfuata mwamuzi baada ya dakika 120 kumalizika akionyesha kutokubaliana na maamuzi yake.
#FIFACWC
#NTTupdates