Na Mwandishi wetu.
Kituo cha Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC) kimeendesha mafunzo kwa viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita kuhusu uibuaji wa miradi inayoweza kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP.
Mafunzo hayo yamejumuisha wakufunzi Dr. Abiud Bongole na Christine Kaigarula, yakifanyika katika Ukumbi mdogo wa Halmashauri ya Manispaa ya Geita.
Dkt. Bongole amesisitiza umuhimu wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP) katika utekelezaji wa miradi, akitolea mfano miradi mbalimbali inayoweza kufanikiwa kwa kutumia mfumo huu.
Amewashauri viongozi wa Manispaa ya Geita kutafuta miradi ya kipaumbele inayoweza kutekelezwa kwa ubia ili kuharakisha maendeleo.
Mafunzo haya ni sehemu ya mpango wa PPPC wa kutoa mafunzo ya uibuaji wa miradi kwa mikoa 13 nchini.
Baada ya mafunzo, wakufunzi hao wanatarajiwa kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na inayotarajiwa kutekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita kwa ajili ya kutoa mwongozo zaidi.
Kituo cha PPPC kinaendelea kufanya kazi na halmashauri na wadau mbalimbali nchini ili kuhamasisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ushirikiano wa sekta za umma na binafsi.
#NTTupdates.