×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

PROF. NDAKIDEMI AGAWA MICHE 10,000 YA MIGOMBA

Na Mwandishi wetu.

Katika kuhakikisha kilimo cha zao la ndizi kinaendelea kuimarisha uchumi wa familia na upatikanaji wake sokoni leo Machi 31, 2025 Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof. Patrick Ndakidemi ametoa jumla ya miche 10,000 ya migomba kwa Kata 14 za Jimbo la Moshi ili kuhakikisha zao hilo linaendelea kupatikana kwa wingi.

Prof. Patrick amegawa miche hiyo kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka katika Kata 14 za Moshi Vijijini ambapo zao hilo limekuwa likilimwa kwa kiasi kikubwa.

Amesema kuwa miche hiyo itasaidia kukuza uchumi wa familia kutokana na uwezo wa miche ya migomba hiyo kuwa na uwezo wa kubebe mkungu wa ndizi wenye uzito wa Kilo 150 hadi 200 kitu ambacho kitawasaidia sana wakulima wa zao hilo wakati wa kufanya biashara hiyo ya ndizi.

Ameongeza kwa kusema kuwa, Kwa sasa Serikali inaandaa mpango maalumu utakaofanya zao la ndizi kuwa zao la kibiashara hivyo wakulima kutoka maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo wanapaswa kunufaika na miche hiyo ili ile dhima iliyokusudiwa iweze kutimia.

#NTTupdates.