Na Mwandishi wetu.
Mabingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa Paris Saint German imeweka rekodi ya kutinga fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) baada ya kupata ushindi wa matokeo ya jumla wa magoli 3-1 dhidi ya Arsenal.
Paris Saint German imetinga hatua hiyo kwa kuziondoa timu nne za ligi kuu ya Uingereza (EPL) ambazo ni Manchester City kwenye hatua ya makundi, Liverpool kwenye hatua ya mtoano, Aston Villa robo fainali na Arsenal kwenye nusu fainali.
PSG hajawahi kushinda taji lolote la ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), licha ya kusajili mastaa kadhaa kwa misimu iliyopita lakini walishindwa kutamba kwenye michuano hiyo.
#NTTupdates