Na Mwandishi wetu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar itapiga hatua kubwa ya Maendeleo endapo kasi iliyooneshwa katika Ujenzi wa Miradi ya Maendeleo itaendelezwa.
Rais Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipoifungua Skuli ya Msingi ya Michakaini ,Wilaya Chakechake ,Mkoa wa Kusini Pemba tarehe 11 Januari 2025.
Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Usimamizi Mzuri wa Miradi ya Miundombinu ya Barabara, Masoko na Skuli za Ghorofa kujengwa Kwa muda uliopangwa ni kasi ya Kupigiwa Mfano Inayopaswa kuendeleza katika Sekta zote.
Amefahamisha kuwa Serikali imeitekeleza Ilani ya CCM kwa Mafanikio makubwa na kuvuka Malengo yaliyomo katika Ilani hiyo katika kipindi cha Miaka Minne.
Akizungumzia Skuli aliyoifungua ya Michakaini amefahamisha kuwa ni hatua muhimu ya Kuwatengenezea Wanafunzi na Walimu Mazingira Mazuri ya Kusomea na kusomeshea.
Amesisitiza kuwa Ilani ya CCM iliitaka Serikali Kujenga Mabanda ya Skuli 1,500 lakini Serikali ya Awamu ya Nane imejenga Skuli za Kisasa za Ghorofa 35 zikiwa na Maabara, Maktaba,Vyumba vya Kompyuta ,Kumbiza kufanyia Mitihani na Vyoo vya kutosha.
Rais Dk.Mwinyi amesisitiza kuwa Serikali Itaendelea kuwapa kazi Wakandarasi waliofanya vizuri katika Miradi ya Maendeleo .
Akijibu Maombi ya Wanànchi wa Jimbo la Chake Chake yaliyowasilishwa na Mbunge na Mwakilishi ya Kujengewa Soko la Kisasa, Skuli nyengine ya Ghorofa na Kituo cha Mabasi , Rais Dk.Mwinyi ameahidi Serikali kuyafanyia kazi maombi hayo aliyoyaelezea kuwa na umuhimu kwa jamii.
Skuli hiyo Imegharimu Shilingi Bilioni 4.1 ina Madarasa 29, Vyoo 25 ,Ukumbi wa Mikutano ,Maabara na Maktaba ina Uwezo wa Kuchukua Wanafunzi 1,305 Kwa wakati Mmoja kwa wastani wa Wanafunzi 45 kila Darasa.
#NTTUpdates