Na Mwandishi wetu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewasisitiza Viongozi wa Dini, Wanasiasa na Waandishi wa Habari kutumia majukwaa yao kutoa kauli nzuri zenye Kuleta Umoja ndani ya Jamii na Amani ya Nchi.
Alhaj Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa iliyofanyika Msikiti Mkuu wa Ijumaa, Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alhaj Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Viongozi wa Dini na Wanasiasa Wawe na kauli zenye kusikilizwa na Watu wengi hivyo ni Vema wakatumia Majukwaa yao kutoa Kauli njema zitakazojenga Umoja ,Undugu, Mshikamano na Amani.
Akiwazungumzia Waandishi wa Habari Alhaj Dk.Mwinyi amewahimiza kutumia Kalamu zao vizuri na kujihadhari na yale wanayoyaandika katika Televisheni ,Redio na Mitandao ya Kijami kuwa hayana Viashiria vya Uvunjifu wa Amani.
Halikadhalika, Alhaj Dk.Mwinyi amefahamisha Kuwa Kwa miaka Mingi iliopita Uzoefu Umeonesha Kuwa Zanzibar ilikuwa ikiingia katika Mifarakano kila Unapofika Wakati wa Uchaguzi jambo lisilopaswa kutokea tena.
Aidha Alhaj Dk. Mwinyi amesema ni lazima Nchi ioneshe kuwa Inaweza kufanya Uchaguzi kwa Amani hatimae ipige hatua zaidi za Maendeleo.
#NTTUpdates