×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RAIS SAMIA AAGIZA UTUNZAJI WA RASILIMALI ZA MAJI

Na Mwandishi wetu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maji na kuboresha huduma rafiki hili kuondoa changamoto kwa wananchi.

Samia ameyasema hayo wakati akizundua mradi wa maji Butimba uliopo mkoani Mwanza huku akibainisha kuwa serikali imedhamiria kutegua kitendawili cha ukosefu wa maji safi na salama yenye kutosheleza kwa wakazi wa jiji hilo.

Amesema ziwa Victoria ni vyema likatunzwa kwa kudhibiti magugu maji ambayo yamekuwa yakikwamisha upatikanaji wa maji safi na Salama na kuzuia zoezi nzima la usafirishaji.

Alitoa maagizo kwa wizara husika na wananchi kwa ujumla kuwekeza nguvu zaidi katika utunzaji wa Mazingira na miundombinu ya maji hili kufanya mradi huo kuwa na tija pasipo kusahau ulipaji wa bili za maji hili kuendeleza mradi huo.

Kwa upande wake waziri wa maji Jumaa Aweso amesema kuwa kiasi cha shilingi Bilioni 71.7 kimetumika hili kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika mkoa huo ambao baadhi ya wakazi wake uishi katika maeneo ya milimani.

Aweso amesema hadi sasa zaidi ya vijijini 10500 vimefikiwa na miradi ya maji kupitia wakala wa usambazaji wa maji vijijini RUWASA lengo ikiwa ni kuondoa hadha ya upatikanaji wa maji katika maeneo ya vijijini.

#NTTUpdates