×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RAIS SAMIA AAHIDI KUENDELEZA MIRADI YA KIMKAKATI

Na Mwandishi wetu.

Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan amesema, kukamilika kwa daraja la JPM Kigongo Busisi linakwenda kufungua fursa za kiuchumi pamoja na kuimarisha biashara za kikanda kwa Maslahi mapana ya taifa.

Rais Samia ameyasema hago wakati wa hafla ya uzinduzi wa daraja hilo na kubainisha kuwa alipokea Mradi huo ukiwa na asilimia 25 pekee huku malengo ya daraja hilo likiwa na lengo la kuunganisha barabara kuu za wakazi wa usagara na Sengerema ili kukuza uchumi wa Kanda ya Ziwa .

Amesema daraja hilo limetumia kiasi Cha Shilingi Bilioni 718 hadi kukamilika kwake huku asilimia 100 ya fedha za gharama zote ni mapato ya ndani ya nchi.

Rais pia amesema ujenzi wa daraja hilo umeongeza maarifa na ujuzi Kwa wakandarasi na ni faida kwa taifa na inaonyesha dhana ya kujitegemea na kusistiza vijana walioshiriki katika Ujenzi huo kuendeleza ujuzi wao katika miradi mingine ya kimkakati.

Amesema kukamilika Kwa Daraja Hilo kunawenda Kuraisisha shughuli za usafirishaji wa abiria na mizigo huku akisisitiza Wananchi kutumia daraja Hilo Kwa manufaa na Kuongeza uzalishaji wa chakula.

Aliwaasa viongozi Kubuni njia rafiki za kukuza mahusiano na majira ili kukuza biashara Kwa wakazi wa mikoa y Kanda ya Ziwa na kuimarisha biashara za kikanda.

Amesema serikali imetekeleza ujenzi wa madaraja tisa yakimkakati ikiwemo daraja la Tanzanite, daraja la Mpwapwa, Daraja la Kigongo JPM Kigongo Busisi na daraja la Kilengule.

Aliagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha kuwa wanalindwa rasilimali zote za daraja hilo hili kuleta tija na Wananchi na madereva kulinda rasilimali hiyo Kwa uzalendo Mkubwa.

#NTTUpdates