×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RAMOVIC ” TUTAJARIBU KILA KITU KESHO ILI KUFIKISHA LENGO LETU”

Na Mwandishi wetu.

Kuelekea mchezo wa kesho wa hatua ya makundi ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) ambao utawakutanisha Vinara wa kunzi Al Hilal Omdurman ya dhidi ya Wananchi Young Africans SC nchini Mauritania Kocha wa klabu ya Young Africans SC, Ramovic ameweka wazi kuwa mchezo wa kesho ni kama fainali kwao ili kutimiza lengo lao la kufuzu hatua ya robo fainali.

“Hatutaki kuwa wa kwanza kupoteza nafasi dhidi ya wapinzani wetu, Kimsingi, tutajaribu kila kitu kesho ili kuona kama tunaweza kufanikisha lengo letu, tunajua kwamba jambo muhimu ni ushindi na tunalichukulia kwa uzito mkubwa.

‘”Mpango wetu uko wazi, tunapaswa kuonyesha kwamba tunaweza kupata magoli na kushinda, Tunacheza dhidi ya timu yenye nguvu kubwa katika eneo la ulinzi kwa hiyo tunapaswa kuwa wabunifu kesho na kujaribu kutumia nafasi zetu vizuri zaidi”

Lazima tuonyeshe ukuaji wetu, tuchukue kila nafasi kwa umakini na tuwe na uthubutu wa kushambulia ili tuweze kutengeneza nafasi ya ushindi.

Wanacheza kwa kasi na tunapaswa kuwa tayari kukabiliana nao.” Maneno hayo yamesemwa na Kocha huyo kwenye mkutano na Waandishi wa habari kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho siku ya Jumapili saa 4:00 usiku.

Young Africans SC inashika nafasi ya tatu kwenye Kundi A ikiwa na alama 4 huku kinara ya Kundi hilo ni Al Hilal Omdurman ambaye amefuzu tayari robo fainali akiwa na alama 10, akifuatiwa na MC Alger ya Algeria yenye alama 8.

#NTTupdates