×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RASHFORD HAKAMATIKI ASTON VILLA

Na Mwandishi wetu.

Kiungo mshambuliaji Marcus Rashford (27) raia wa Uingereza, anayekipiga kwa mkopo kwenye klabu ya Aston Villa akitokea Man United ameendelea kuonyesha makali yake ndani ya kikosi hicho ndani ya muda mfupi toka ajiunge nao.

Rashford ambaye amekuwa na mwanzo mzuri ndani ya Aston Villa huku Kocha wa kikosi hicho Unai Emery akiweka wazi kuwa ni mchezaji mzuri na huenda wakamsajili moja kwa moja kutokea Manchester United.

Rashford mpaka sasa amechangia magoli 7 kwenye michezo 6 toka ajiunge na kikosi Cha Aston Villa dirisha dogo la usajili huku klabu yake ya Manchester United ikiendelea kuwa na matokeo ya kusuasua kwenye ligi kuu EPL.

#NTTupdates