Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amekutana na timu ya wataalam kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Ofisini kwake Ilala Boma.
RC Chalamila pamoja na mambo mengine alipata wasaa wa kufanya mazungumzo na timu hiyo ikiongozwa na Kamishna wa Bima Dkt Baghayo Sakware ambapo kwa pamoja walijadili namna bora za kuweza kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwa Bima za aina mbalimbali katika maisha ya kila siku.
Aidha RC Chalamila ameitaka mamlaka hiyo kuendelea kuhamasisha na kutoa elimu ya Bima katika makundi mbalimbali ikiwemo kundi la wafanyabiashara wakubwa na wadogo pia watumishi wa umma na binafsi ili kuleta uelewa mpana wa Bima kwa jamii.
Sanjari na hilo timu hiyo imewasilisha ombi kumuomba, Mkuu wa Mkoa kuwa Balozi wa Bima, vilevile wamewasilisha ombi la kuandaliwa kikao na kundi la Viongozi na watumishi wa Mkoa huo pamoja na kundi la wafanyabiashara ili kuweza kuhamasisha makundi hayo umuhimu wa Bima na kutoa elimu ya Bima.
#NTTupdates