×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RC MAKALLA ATOA ONYO KWA VIJANA WANAOPORA MALI ZA WANANCHI ARUSHA

Na Mwandishi wetu.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha,CPA. Amos Gabriel Makalla, ametoa onyo kwa vijana wanaotumia usafiri wa pikipiki kufanya uhalifu mkoani Arusha, maarufu kama tatu mzuka, kuacha mara moja vitendo hivyo badala yake kutafuta kazi nyingine halali ya kufanya.

CPA. Makalla ametoa onyo hilo leo Oktoba 13, 2025 kufuatia malalamiko ya wananchi wa kata ya Muriet wakati akitembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Stendi Kuu ya mabasi ya mkoa wa Arusha, kata ya Muriet.

“Tatu mzuka popote walipo, natoa onyo kuachana na uhalifu wa kutumia pikipiki, nasema wasinichokoze, nitakula nao sahani moja, mkoa wa huu unahitaji kuwa salama, nikiwa mkuu wa mkoa ni marufuku Tatu Mzuka, nawaonya watafute kazi nyingine” Amesema CPA Makalla

Aidha, amewasisitiza vijana hao wa maarufu kama tatu mzuka kutambua kuwa mkoa wa Arusha una wageni wengi kutoka ndani na nje ya nchi hivyo, hivyo kila mwananchi anatakiwa kufanya kazi halali pamoja na kuwa mlinzi wa usalama wa eneo lake na sio kufanya uhalifu na kuonheza kuwa Arusha inahitajika kuwa salama zaidi.

#NTTupdates.