Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, amewataka Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa usambazaji umeme wa jua katika maeneo 39 ya Visiwa vya Mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanatekeleza miradi hiyo kwa wakati li kuondoa hadha ya ukosekanaji wa nishati ya umeme wa uhakika katika maeneo hayo.
Mtanda ameyasema hayo Wakati akizungumza na Wakandarasi na Wataalamu kutoka Wakala wa Umeme Vijijini (REA) huku akiwataka Wakandarasi kujitambulisha katika ngazi zavijiji, tarafa na Wilaya ambazo mradi huo utatekelezwa ili kupata taarifa, maoni na mapendekezo ya namna ya ufanikishaji wa zoezi.
Hilo lengo likiwa ni kuleta uelewa wa pamoja Kwa Wananchi ambao ni wanufaika wa Mradi huo.
Kwa upande wake Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Ziwa Mhandisi Ernest Makale amesema mradi huo utatekelezwa katika Wilaya za Sengerema, Buchosa, Ukerewe, Magu na Ilemela ambapo tayari fedha zaidi ya bilioni 4 zimeshatengwa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo huku inakadiriwa nyumba 8410 zitafikiwa na kutakua na mgawanyo wa njia 8 lengo likiwa ni kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati kama ulivyopangwa.
Alitoa wito Kwa Wananchi kuchangamkia mradi huo pale utakapoanza kutelekezwa na ata Mara baada ya kukamilika maana malengo ya REA ni kuondoa changamoto za Umeme Kwa wakazi wa maeneo ya visiwani ili waweze kutekeleza shughuli zao za uzalishaji Mali Kwa urahisi.
#NTTUpdates