×
New Times Tanzania New Times Tanzania is a multi-media organization with investments in media platforms spanning newspaper print operations, television, radio broadcasting, digital and online services.
New Times Tanzania

RC MTANDA ATOA MBINU YA KUONGEZA UFAULU MASHULENI

Na Mwandishi wetu.

Wazazi, Walezi na wadau wa elimu Kwa ujumla Wametakiwa kushirikiana na waalimu mashuleni Katika kusimamia wanafunzi shuleni ili waondokane na utoro na tabia hatarishi zinazopelekea baadhi ya wanafunzi wa kike kupata ujauzito wawapo masomoni.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda wakati wa hafla fupi ya utoaji tuzo na zawadi Kwa shule na Wanafunzi waliofanikisha matokeo bora kitaalamu Katika mitihani ya elimu ya msingi na sekondari pamoja na michezo Kwa kipindi Cha mwaka 2024 na 2025.

Mkoani humo ambapo wilaya ya Ilemela iliibuka mshindi wa jumla Mtanda amesema kuwa jamii inalojukumu la Kuhakikisha watoto wanakuwa Katika misingi na maaduli bora kwa maslahi ya ujenzi wa taifa lenye viongozi imara waliolelewa vyema.

Katika atua nyingine alisema kuwa ushirikiano mzuri baina ya Wazazi, walezi, Waalimu na Wanafunzi ndio chachu ya matokeo chanya katika Sekta ya elimu kwenye mitihani ya kitaifa inayosimamiwa na Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania(NECTA).

Mtanda amebainisha kuwa mwaka 2024 Mwanza imefanya vizuri katika mitihani ya NECTA ukilinganisha na 2023 ambapo kwa Darasa la Nne ufaulu ulikuwa 83% hadi 91%, Kidato cha Pili 87% hadi 89% Darasa la Saba 84% hadi 85%, Kidato cha nne 94% hadi 98% na Kidato cha Sita 2024 99.6% hadi 99.83 2025.

Aidha, ameeleza kuwa matokeo ya mitihani ya 2024 sio tu kwamba yameufanya Mkoa huo kufaulisha bali kutambulika kitaifa kwa kushika nafasi ya Sita kwa Elimu Msingi na nafasi ya Tatu kwa sekondari na kwamba kwa upande wa michezo Mkoa umeshika nafasi ya Kwanza kwa mara nne mfululizo.

#NTTupdates