Na Mwandishi wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameigiza Shirika la Uwakala wa Meli (TASAC) kutoa elimu kwa Wananchi na Wakazi wa Kanda ya Ziwa kwa ujumla juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uokozi wa majini hili kusaidia kuokoa uhai wa watu wanapopata majanga ya majini.
Mtanda ametoa kauli hiyo wakati akikagua Boti ya Uokozi(AMBULANCE BOAT) katika bandari ya Mwanza Kaskazini ambapo amesema kuwa awamu hiyo ni ya kwanza huku akisisitiza kuwa kuwaelimisha watu kujua Umuhimu wa kushirikiana na serikali, kutoa taarifa na kushiriki katika uokozi pale zinapotokea ajali za majini itasaidia kuokoa uhai wa watu wengi kupitia ushiriki wao.
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda Kaimu Mfawidhi wa Shirika la Uwakala wa Meli(TASAC) Mwanza, Joseph Mkumbo amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya taratibu za maandalizi ya kukabidhiwa boti hiyo Kutoka Kwa mjenzi wa boti na mara baada ya makabidhiano hayo ofisi ya Mkuu wa Mkoa itapewa mualiko maalumu.
Naye Mkurugenzi wa Meli za Ndani na Njee TASAC, Nahodha Grayson Marwa amesema kuwa madhumuni makuu ya boti hiyo ni kwaajili ya matibabu ndani ya maji na kutoa msaada wa uokozi pale zinapotokea dharura za majini.
Ameongeza kuwa boti hiyo ni ya kisasa inayo mwendo wa kasi na ni hospitali inayotembea kwani inao uwezo wa kulaza wagonjwa wanne pamoja na watoto lakini pia inayo uwezo wa kuzalisha hewa ya oksijeni kwa watu wenye tatizo la upumuaji pamoja na kufanya upasuaji mdogo ikiwa Kuna mtu amepata ugonjwa wa dharura pamoja na uzazi.
Ujenzi wa boti hiyo umefanyika nchini Uturuki na umegharimu Kiasi cha shilingi Bilioni 4.25 kwajili ya kutoa msaada wa uokozi wa majini kwa Wakazi wa Kanda ya Ziwa.
#NTTupdates